Pages

Tuesday, August 12, 2014

KAMPUNI YA MAFUTA NA GESI YA SWALA YAKARIBISHWA RASMI SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akigonga kengele kuashiria kuingia rasmi kwa kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. David Mestres akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukaribishwa rasmi kwa kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam.

Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa sherehe za kukaribishwa rasmi kwa kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam.

Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipozi kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. Ernest Massawe(kushoto) na Mkurungenzi wa Swala Bw. Abdullah Mwinyi kwenye sherehe za kukaribishwa rasmi kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam.

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi na Mhe. Joseph Mungai wakimsikiliza Rais Mstaafu Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa kukaribishwa kwa kampuni ya Swala kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi  akifurahia jambo na Mkurungenzi wa Swala Bw. Abdullah Mwinyi.

No comments: