![]() |
Marehemu Dkt William Mgimwa, enzi za uhai wake. |
MWILI wa Waziri wa Fedha, Dkt William Mgimwa unatarajiwa kuwasili nchini kesho mchana kwa ndege ya Afrika Kusini.
Utaagwa keshokutwa katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa Jumatatu kwenda kuzikwa kijijini kwake Magunga, wilaya ya Iringa Vijijini.
Akitoa taarifa kuhusu mazishi, Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi kitaifa, William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Utaratibu na Bunge) alisema mwili utapokewa kesho saa 7 mchana katika uwanja wa ndegewa Julius Nyerere, terminal II.
Lukuvi alisema baada ya hapo, mwili utapelekwa nyumbani kwake Mikocheni B na saa 11 utapelekwa hospitali ya Lugalo utakapolala.
Alisema Jumapili saa 3.00 hadi 4.00 asubuhi kutakuwa na chakula nyumbani kwa marehemu kisha saa 4.30 mwili utawasili nyumbani kwake kutoka hospitali kabla ya kupelekwa Karimjee kwa ajili ya ibada na heshima za mwisho.
Baada ya kuagwa, mwili utapelekwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, terminal II na kusafirishwa kwa ndege ya serikali kwenda mkoani Iringa kwa maziko.
Inatarajiwa saa 10.00 jioni mwili utawasili katika kiwancha cha ndege cha Nduli na kupokewa na wananchi wa mkoa huo, ambako mipango ya maziko inafanya na kamati ya mkoa inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa, Dkt. Christine Ishengoma. Utaagwa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo, ambako marehemu Dkt. Mgimwa inaelezwa alifanya kazi kwa muda mrefu.
"Baadaye saa 11.30 jioni (Jumapili) mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea kijijini kwake, Magunga utakapolala na siku inayofuata yaani Jumatatu saa sita mchana shughuli za maziko zitaanza kijijini hapo," alisema Lukuvi.
Kwa mujibu wa Lukuvi, Kamati ya Maziko imejumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Afya, Bunge, Ikulu, Mambo ya Nje na ndani na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kuhusu tatizo lililosababisha kifo, Waziri Lukuvi alisema zitaelezwa katika ukumbi wa Karimjee wakati wa shughuli ya kumuaga. Wakati huo huo Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za rambirambi Rais Jakaya Kikwete kutokana na kifo cha Waziri Mgimwa.
Katika salamu zake, Dkt Shein alisema daima atakumbukwa kutokana na utumishiwake uliotukuka kwa serikali na wananchi wa Tanzania.
"Tanzania imempoteza kiongozi shupavu, mpenda kazi, mzalendo na mtu mwenye busara na upendo kwa wenzake," alisema Dkt Shein kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

CHANZO: Habari Leo
No comments:
Post a Comment