MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo
haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul (Diamond
Platnumz) kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi
wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu
ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi
amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko
kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,”
Alisema na kuongeza .
“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu
umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata
rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka
nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.”
Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA,
na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope.
Alisema. Awali akifungua semina hiyo. Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari
kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA,
katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa
huduma stahiki kwa wananchi.
“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto
nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili
kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe
kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu
kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo.
Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka
ya kukusanya kodi za serikali kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za
umma.
“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi
watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii
waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi
ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.


Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia),
akiwakaribisha waandishi wa habari kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa
semina, Bi. Angella Msangi.

Mkutano huo ukiendelea.

Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
No comments:
Post a Comment