Marehemu John Mabula, enzi za uhai wake. |
Aliyewahi kuwa mchezaji mpira wa timu ya Mtibwa Sugar miaka ya 2002, John Mabula ameuawa kwa kuchomwa kisu maeneo ya Kitunda, Dsm alipokuwa akiamulia ugomvi wa shemeji yake.
Katika tukio hilo la kusikitisha, shemeji yake huyo ambaye ni mdogo wa kiume wa mkewe nae pia aliuawa kwa kuchomwa visu na muuaji huyo ambaye bado hajafahamika.
Akielezea tukio hilo, jirani wa marehemu amesema kuwa mke wa marehemu John alimgongea nyumbani kwake usiku wa manane huku akiwa na damu mwilini mwake.
"Mida ya kama saa nane usiku jirani yangu alinigongea akiniomba nimfungulie atauliwa, ndipo nikamfungulia na kumkuta akiwa na damu na akanieleza kuwa nikamsaidie mumewe na mdogo wake wanauliwa na mtu katika grocery ya jirani"
Jirani huyo aliendelea kueleza kuwa waliamua kwenda kwa mjumbe ambaye waliongozana nae hadi eneo la tukio ambapo walikuta maiti zote mbili zikiwa pale peke yake huku watu wengine wote wakiwa wameondoka.
vifo vya marehemu hao vimeelezwa kutokea kutokana na ugomvi ambapo marehemu John pamoja na mkewe na Shemeji yake walikuwa katika bar iliyopo karibu na nyumbani kwao. Shemeji (mdogo wa mke wa John) alitoka kwenda msalani ambapo kabla ya kufika alikwenda sehemu ya runinga na kuzuia watu wengine wasitizame ndipo ugomvi ukaanzia hapo watu wakaanza kumzonga na akatokea jamaa mmoja wakaanza kurushiana maneno na kupigana ndipo John akaingilia kutaka kuwaamulia jamaa kuona hivyo akachomoa kisu kwenye kibegi chake na kuanza kumchoma mgomvi wake baada ya hapo akamchoma na John.
Watu wote walianza kutawanyika kwa hofu na huyo mtu alimfuata mke wa John kutaka amchome visu pia lakini mwanamke huyo alimuomba msamaha sana akimtaka asimuue ambapo mtu huyo alimkata visu mkononi na kumwamuru aondoke haraka eneo hilo.
Baada ya hapo muuaji akaondoka zake na mpaka sasa hajajulikana alipotokomea muuaji huyo.
Miili ya Marehemu imesafirishwa leo ambapo John anapelekwa Shinyanga na Shemeji yake anapelekwa Mwanza.
Chanzo: Clouds FM/ Heka heka

No comments:
Post a Comment