Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria. |
Rais
wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa serikali yake imepigwa na
butwaa na matamshi ya kushtua na ya aibu ya Waziri Mkuu wa Uingereza Bw
David Cameron ya kwamba Nigeria na Afghanistan ndio mataifa fisadi zaidi
duniani.
Rais Buhari ameyasema hayo muda mchache tu baada ya kupata habari hiyo kuhusu Waziri Mkuu huyo.

Garba Shehu ambaye ni msemaji wa Rais huyo ametaja matamshi ya Cameron kuwa ni ya aibu na kushtua na kwamba Rais Buhari ndiye haswa fagio la ufisadi nchini humo.
"Labda Cameron alikuwa akizungumzia utawala wa Goodluck Jonathan ulioondoka madarakani mwezi Mei mwaka jana. Buhari alichaguliwa kwa jukwaa la kupambana na ufisadi na yeye ndiye kifagio cha ufisadi nchini Nigeria," amesema Shehu.
Malkia Elizabeth (kushoto) akimsikiliza Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron (kulia) huku Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby (katikati) akifuatilia maongezi hayo. |
"Asisahau kuwa Rais
Buhari alialikwa katika kongamano hilo huko London kutokana na jitihada
zake ngangari za kupigana na ufisadi, itakuwaje awe fisadi," aliuliza
bwana Shehu.
Muda mchache uliopita, habari zimeibuka zikimuonesha Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron aliyenaswa na kamera katika dhifa ya kusherehekea miaka 90 tangu kuzaliwa kwake Malkia Elizabeth akimwambia Malkia kuwa viongozi wa nchi za Afghanistan na Nigeria ambazo ndio mataifa yenye ufisadi zaidi duniani watahudhuria kongamano.
''Viongozi wa mataifa mafisadi wakuu duniani wakiwemo viongozi wa Afghanistan na Nigeria mataifa yanayoorodheshwa kuwa mafisadi zaidi kote duniani watakuwa nchini uingereza siku ya Alhamisi kuhudhuria kongamano la kutathmini mbinu za kukabiliana na zimwi la ufisadi.'' amesema Cameron.
Kiongozi wa Kanisa la kianglikana Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby aliyekuwa na viongozi hao wawili anaonekana akimkumbusha bw Cameron kuwa Rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari si fisadi.
Chanzo: BBC Swahili

No comments:
Post a Comment