Msanii Snura Mushi. |
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo leo imetangaza kuufungia wimbo na video ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi unaofahamika kwa jina la 'CHURA' kutokana na
kutokuwa na maadili ya Mtanzania.
Wimbo huo pia umezuiwa kutumbuizwa mahala popote na kufungiwa kuchezwa kwenye redio na runinga nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha
mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza
wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp na Instagram na
kuongeza kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia
sheria ya makosa ya mtandao.
Pia Wizara hiyo, imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya msanii huyo, mpaka pale atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake zote kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Serikali imewataka wanasii mbalimbali nchini, kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za sanaa.
No comments:
Post a Comment