Klabu ya soka ya Atletico Madrid
imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya
pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini
walipokipiga dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Atletico wakiwa
na faida ya bao la nyumbani katika nusu fainali ya kwanza nchini
Uhispania, Bayern walisawazisha kupitia mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa
na Xabi Alonso kwenye mechi ya Jumanne iliyochezewa uwanja wao wa
nyumbani wa Allianz Arena.
Mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak
aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Thomas Muller kabla ya
mshambuliaji Antoine Griezmann kusawazisha na kuwa 1-1.
Robert Lewandowski alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ya
mpira wa kichwa kutoka kwa Arturo Vidal huku Atletico wakishindwa
kusawazisha baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Fernando Torres
kuokolewa na mlinda mlango Manuel Neuer.
Matokeo ya jumla ya nusufainali hiyo yalimalizika sare 2-2 lakini Madrid wakasonga kwa kuwa na bao la ugenini.
Sasa
Atletico watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na
Manchester City utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu katika
fainali mjini Milan tarehe 28 Mei.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment