Pages

Monday, September 9, 2013

"NDUGAI ALITUMWA NA NEC KUHAKIKISHA MATAKWA YA CCM YANATIMIA BUNGENI" - MNYIKA


Mhe John Mnyika (Mb) katika kipindi cha "Tuongee Asubuhi" ndani ya Star TV ameeleza kuwa Naibu Spika mhe Ndugai aliagizwa na NEC kihakikisha matakwa ya CCM yanapita katika Katiba, hivyo alichokua anafanya bungeni juzi ni kutekeleza maagizo.

Pia kasema askari walioingia kuleta fujo bungeni waliandaliwa kabisa na wengine hata si askari wa pale bungeni na ana ushahidi akitakiwa kuutoa maana anawafahamu kwa sura na majina (akimaanisha ilipangwa mapema liwalo na liwe lakini matakwa ya wapangaji yatimie).

Amezungumza mengi machache ya hayo ni kuonyesha jinsi gani Zanzibar hawajashirikishwa (na yeyote anaesema wameshirikishwa ni mwongo), upinzani walichokuwa wanakifanya ni "filibustering".

Pia akamalizia kwa kusema hatua inayofuata ni kurudi kwa wananchi wao ndio waamue muafaka wa Katiba mpya "nguvu ya umma."

Source: eddymoblaze blog

No comments: