Pages

Monday, September 9, 2013

MELI ILIYOKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA KATIKA BAHARI YA MEDITERRANEAN ILISAJILIWA ZANZIBAR

Mmea wa bangi.

POLISI nchini Tanzania wamethibitisha kuwa meli iliyokamatwa Jumamosi katika bahari ya Mediterranean ikiwa na mizigo ya bangi yenye thamani ya dola milioni 78 ilikuwa imesalijiliwa Zanzibar.

Wafanyakazi tisa waliokuwa kwenye meli hiyo wanaosemekana kuwa raia wa Misri na Syria, waliiwasha moto meli hiyo na kuruka baharini, ingawa baadaye waliokolewa.

Maafisa wa ushuru wa Italia walioinasa meli hiyo iliyokuwa kwenye ufukwe wa Sicily baada ya kupata taarifa, walisema kuwa mizigo ya bangi yenye tani 30 ilipakiwa kwenye meli hiyo katika bandari ya Uturuki ingawa haijulikani mzigo huo ulikokuwa unapelekwa.

No comments: