Pages

Thursday, August 29, 2013

WABUNGE WA TANZANIA EAC WATOKA NJE YA KIKAO KUPINGA HOJA; KIKAO CHAVUNJIKA

 
Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wakitoka ndani ya ukumbi wa Bunge hilo jana kupinga wabunge wenzao wanaoshinikiza hoja ya vikao vya Bunge kufanyika kwa mzunguko kwa nchi zote zinazowasilishwa bungeni hapo. Kutoka kushoto ni Mhe. Twaha Taslima, Mhe. Shyrose Bhanji, Mhe Abdullah Mwinyi na
Mhe. Nderakindo Kessy.

 Mbunge wa Tanzania ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mhe. Abdullah Mwinyi (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baada ya kutoka nje ya kikao kupinga shinikizo la hoja ya wabunge wenzao ya vikao vya Bunge kufanyika kwa mzunguko/zamu katika nchi zote zinazowakilishwa na Bunge hilo.  Kikao hicho kiliahirishwa hadi leo. 
Wa pili kulia ni mwandishi Zephania Ubwani.

No comments: