Pages

Thursday, August 29, 2013

REDD'S MISS TANZANIA 2012/2013, BRIGITTE ALFRED AAGWA RASMI JIJINI DSM

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wakuu wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kushoto) akimuaga rasmi Redd's miss Tanzania 2012/2013, Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mhe. Fenella Mukandara (kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga mrembo huyo iliyofanyika jana katika hoteli ya Giraffe jijini DSM.

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukandara (kulia) akimkabidhi Bendera ya taifa Redd's Miss Tanzania 2012/2013, Brigitte Alfred (katikati) anayetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki katika shindano la urembo wa dunia (Miss World 2013).  Kushoto ni mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania, Emmanuel Ole Naiko.

Brigitte Alfred, Redd's Miss Tanzania 2012/2013 akiongea na wageni waalikwa waliofika katika hafla yake ya kuagwa iliyofanyika jana usiku jijini DSM katika ukumbi wa Giraffe Hotel.

 
 
Redd's Miss Tanzania 2012/2013 Brigitte Alfred (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mama yake mzazi katika hafla ya kumuaga iliyofanyika jana usiku jijini DSM.

No comments: