Pages

Wednesday, August 21, 2013

REDIO ZA KIJAMII NCHINI ZATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA KUTENGENEZA VIPINDI VITAKAVYOIGUSA JAMII MOJA KWA MOJA

Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jinsi waandaaji wa vipindi wanavyoweza kutafuta habari nzuri zenye kuelimisha kwa ajili ya redio za jamii na pia mbinu wanazoweza kutumia ili kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
 Mtaalam wa Kilimo kutoka Idara ya Kilimo wilayani Sengerema Bw. Joseph Manota akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari wa redio za jamii inayofanyika mkoani Mwanza ambapo fursa zinazopatikana katika sekta ya Kilimo na jinsi ya kuzitumia ili kufanikisha sera ya Serikali ya Kilimo Kwanza na pia amezungumzia changamoto zilizopo katika kutimiza sera hiyo na namna gani maafisa wa Kilimo pamoja na Serikali kwa ujumla wanaweza wakafanya kukabiliana nazo ili kutimiza malengo ya kukuza Kilimo.
 Mshauri wa redio za jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
 Pichani juu na chini ni waandishi na maripota wa redio za jamii wanaohurudhuria mafunzo hayo yanayofanyika kwenyen kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

 Mwezeshaji kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mtaifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa ambayo yatawasaidia katika kuandika habari zao kiufasaha.
 Mmoja wa watangazaji wa Redio Kahama FM William Bundala (Kijukuu cha Bibi K) akitoa mrejesho wa mafunzo yaliyopita ambayo yameleta mabadiliko makubwa kwa kituo chao kwa Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu

 Afisa Elimu, Takwimu na Vifaa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Pius Lwamimi akizungumza na waandishi wa habari na maripota wa redio za jamii nchini ambapo aligusia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta Elimu wilayani humo na kuwaasa kutumia redio zao katika kutoa taarifa muhimu kwa jamii zitakazopelekea kukua kwa Sekta ya Elimu nchini. Pia amewataka wazazi kuwa mstari wa mbele na kujitokeza kuhudhuria vikao katika shule na kutoa maoni yao kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mitaala ya elimu na pia kushirikiana na redio za jamii kwa kutoa taarifa muhimu na pia kuwahamasisha watoto wao na jamii nzima kujenga utamaduni wa kusikiliza vipindi vya redio hizo kwa manufaa yao.




No comments: