Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton akizungumza na wanachama wa Upendo Hisa Group alipotembelea kikundi hicho kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Miradi wa Shirika la kimataifa la Plan International Bw Paul Lusato na Catherine French Mkuu wa wafanyakazi ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Barclays.
Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton pia alitembelea moja ya saluni ya kutengenezea nywele ya Bi Zainabu Rashidi (kulia) ambaye ni mmoja wa wanakikundi cha Upendo Hisa Group cha Vingunguti Mtambani, DSM.
Kikundi cha ngoma cha Mshikamano kikitumbuiza katika ziara ya Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton (hayupo pichani).
Baadhi ya wakazi wa Vingunguti Mtambani wakimsubili Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton (hayupo pichani).
Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton akitembelea baadhi ya mitaa ya Vingunguti kwa Mtambani jijini Dar es Salaam.
Rais Clinton akisalimiana na wakazi wa Vingunguti Mtambani baada ya kujionea shughuli za Upendo Hisa Group kilichopo maeneo hayo. ( PICHA ZOTE NA IPSHA BLOG)
No comments:
Post a Comment