Pages

Saturday, August 3, 2013

RAIS KIKWETE AFUTURISHA WASANII WA BONGO FLEVA IKULU JANA

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya  Mwasiti Almasi (kushoto) na Zuwena Mohammed a.k.a. Shilole (kulia) wakiwa na mtangazaji wa redio ya Clouds FM Fatma Hassan a.k.a Dj Fetty wakipakua futari kufuatia mwaliko wa Rais Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
1a


Rais Kikwete akisalimiana na msaanii wa kizazi kipya, Chege Chigunda na wenzake wakati alipowaalika kufuturu Ikulu jana jioni.

Mke wa Rais, Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa bongofleva mara baada ya kufuturu.  Kutoka kushoto ni Snura, Keisha, Mwasiti, aliyechuchumaa ni Shilole, DJ Fett (mtangazaji wa radio Clouds FM), Mwanahawa Abdul a.k.a Queen Doreen.
Rais Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa bongofleva Ally Kiba (kushoto) na mdogo wake Abdul Kiba.

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa bongofleva Shilole.
Rais Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmoja wa watangazaji wa redio ya Clouds FM, Mbwiga wa Mbwiguke (kulia).

No comments: