Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando (katikati), Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Mrisho Milao (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel, Bi. Aneth Muga (kulia) wakisubiri droo ya kutafuta mshindi itafute namba ya mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kumsaka mshindi wa nyumba ya kwanza kupitia promosheni ya Airtel Yatosha.
AIRTEL Tanzania imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba kupitia promosheni yake ya Airtel Yatosha Shinda nyumba inayoendelea na kuwazawadia wateja wake kila siku.
Bw. Silvanus Juma mkazi wa Iringa mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni Mhasibu katika Shirika la Tanzania Rural Women and Children Development Foundation (TARWOC) ameibuka mshindi na kuzawadiwa nyumba ya kisasa iliyojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel Bw. Jackson Mmbando alisema "kama tulivyowatangazia awali leo ndio ile siku muhimu na maalumu ya kumpata mshindi wetu wa kwanza wa nyumba na tumeshuhudia Bw. Silvanus Juma akiibuka mshindi kupitia droo ya kwanza tuliyoichezesha hapa.
Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi, Bw. Silvanus Juma amesema "ninayo furaha sana kupata zawadi hii kubwa kutoka Airtel na napenda kutoa wito kwa watanzania na wateja wa Airtel kuendelea kutumia huduma ya Airtel Yatosha na waamini kuwa hakuna upendeleo. Binafsi sijawahi kushinda bahati nasibu yoyote na nilikuwa siamini kama hakuna ubaguzi kwenye kushinda, lakini leo nashuhudia kwamba hakuna ubaguzi na kuwasisitiza wateja wengine wajaribu nao wanaweza kushinda."
Airtel inaendelea na promosheni ya Airtel Yatosha Shinda Nyumba Tatu ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake na kutoa huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel Yatosha.
Sambamba na hilo, Airtel pia inawawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa bure bila makato yoyote.
No comments:
Post a Comment