Pages

Tuesday, April 9, 2013

USANGU LOGISTICS WALAZIMIKA KUNYANYUA MIZIGO KWA KUTUMIA WATU KUTOKANA NA KUTOKUWA NA CRANE



Picha ya juu na chini ni baadhi ya watu ambao walijitolea kupakia contena la mizigo katika gari la mizigo kutoka Zambia ambalo inasemakana magari hayo yalikaa katika yadi ya kampuni ya Usangu Logistics zaidi ya siku 21. Zoezi hilo limefanyika kwa sababu ya kukosekana kwa crane ya kunyanyulia mizigo katika yadi hiyo.


Mmoja wa madereva kutoka Zambia aliyejulikana kwa jina moja la Karume akisubiri gari
lake lipakie mzigo  ili aweze kuondoka nchini baada ya kukaa kwa muda mrefu.
Mkurugezi wa Usangu Logistics akiongea na Wanahabari kuhusu sababu za kutumia watu badala
ya crane  kunyanyua mizigo katika yadi yake iliyopo Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam.
 

Badhi ya wafanyakazi walioshiriki katika kunyanyua contena baada ya kazi hiyo nzito.
                   
Gari la Zambia likiwa linamalizia kupakia mzigo wa contena kwa kutumia watu badala ya
mashine maalumu




Mkurugenzi wa Usangu Logistics Bw Ibrahim Ismail akielezea jambo kuhusu tukio hilo
ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu.


MAGARI  MAKUBWA YA MIZIGO MIZITO KUTOKA ZAMBIA YAPO HAPA NCHINI KWA ZAIDI YA SIKU 21 SASA YAKISUBIRI KUPAKIA SHEHENA YA MIZIGO AMBAYO IMETOKA BANDARINI KUTOKANA NA  MSAFIRISHAJI WA MIZIGO HIYO KUKOSA 'CRANE' YA KUPAKIA NA KUPAKUA MIZIGO JAMBO AMBALO LIMELALAMIKIWA NA MADEREVA WANAOENDESHA MAGARI HAYO KUDHOHOFISHA UCHUMI WAO KUTOKANA NA KUKAA HAPA NCHINI BILA SABABU YOYOTE YA KIMSINGI.
 
WAKIZUNGUMZA JIJINI DAR ES SALAAM MADEREVA HAO WAMESEMA KUWA PAMOJA NA KAMPENI ZA SERIKALI ZINAZOENDELEA KUHUSU SUALA LA KUTOKOMEZA URASIMU WA MIZIGO KUCHELEWA KUTOKA BANDARINI, ENDAPO TATIZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA UPAKIAJI NA USHUSHAJI WA MIZIGO KWA WAKATI KWA WASAFIRISHAJI HALITOSHUGHULIKIWA KWA HARAKA SERIKALI ITAKUWA HAIJAWASAIDIA KUTATUA TATIZO LAO LA KUKAA KWA MUDA MREFU NCHINI PINDI WANAPO TUMIA BANDARI YA DAR ES SALAAM .
 
WAKIZUNGUMZIA TATIZO HILO BAADHI YA WASAFIRISHAJI WA MIZIGO WAMESEMA KUTOKANA NA MAGARI YAO YA KUSHUSHA NA KUPAKIA SHEHENA CRANE KUSHIKILIWA NA WAKALA WA BARABARA NCHINI-TANROAD KUFUATIA UTEKELEZAJI WA SHERIA ILIYOWEKWA NA MAMLAKA HUSIKA YA KUWATAKA WAWE NA VIBALI MAALUMU VINAVYORUHUSU MAGARI HAYO KUTEMBEA BARABARANI ,INAWAPASA KUTUMIA MUDA MREFU KATIKA UTENDAJI NA MARA NYINGINE INAWALAZIMU KUTUMIA WATU BADALA YA CRANE KUPAKIA MIZIGO NJIA AMBAYO SI SALAMA NA INAWEZA KULETA MAAFA.    








No comments: