Pages

Monday, April 15, 2013

MAKAMU WA RAIS DAKTA BILAL ASHIRIKI SHUGHULI YA KUUAGA MWILI WA MEJA JENERALI MAKAME RASHID


Inspekta Jenerali wa Polisi - IGP Said Mwema (katikati) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza, (CGP) John Minja (kulia).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.

Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mkuu wa Majeshi (CDF), Davis Mwamunyange.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame,
zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya
 JKT jijini Dar es Salaam. 


Mkuu wa Majeshi nchini (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange akitoa heshima za mwisho.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal (mwenye suti nyeusi kulia) akiwafariji wafiwa.

Rais mstaafu, Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho.

No comments: