Pages

Wednesday, March 6, 2013

RAIS WA VENEZUELA HUGO CHAVEZ AFARIKI DUNIA


Marehemu Hugo Chaves, enzi za uhai wake.

Makamu wa rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, mwenye umri wa miaka 58, kifo kilichotekea kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez alikuwa anatibiwa kwa muda mrefu nchini Cuba.

Mwezi wa pili rais Chaves alilejea mjini Caracas kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie na kupelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea na matibabu.  Rais Chavez amekua kiongozi wa nchi hiyo kwa miaka 14 ambapo taarifa kutoka kwa jeshi la nchi hiyo zimesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha usalama na kuaihidi kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na kutoa wito kwa raia kuwa watulivu.

Chavez aliingia katika medani ya siasa toka mwaka 1992 akiwa luteni katika jeshi na kuongoza mapinduzi dhidi ya rais Carlos Andres Perez lakini kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa kunyakua madaraka hayo ambapo alikiri kushindwa na aliwekwa kizuizini.

Ushindi mkubwa alioupata chavez mnamo mwaka 1999 ulimweka madarakani ambapo baada ya kuapishwa Chavez alisema kuwa mipango yake ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu ambapo pia alibadili muundo wa bunge na kulifanya kuwa la kikatiba, ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura ya maoni iliyoidhinishwa kwa asilimia 88 ya wapiga kura.

Rais Chavez alitaifisha rasilimali ikiwemo rasilimali kubwa ya mafuta, ambapo sera hizo zilimfanya azozane na makampuni ya kimataifa ya mafuta, jambo ambalo liliungwa mkono hususani kwa watu maskini.

Kutokana na urafiki wake na viongozi wa mrengo wa kushoto kama vile rais wa Cuba, Fidel Castro, ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu aligongana kidiplomasia na Marekani, ambayo ni mshirika wake mkuu wa kibiashara.

Chavez alipendwa nyumbani na wafuasi wake lakini alipingwa na baadhi ya watu nchini humo na katika nchi za nje.  Alionekana sio tu kama bingwa wa jamii maskini lakini pia kama muingiliaji wa siasa za nchi jirani. Katika miaka ya hivi karibuni alilenga kukabiliana na masuala ya ndani ya Venezuela, kama uhalifu, kuinua uchumi wa nchi na kukabiliana na rushwa.

Picha za baadhi ya  waombolezaji nchini Venezuela






Picha na story kwa hisani ya mtandao wa BBC Swahili (www.bbc.co.uk/swahili)

No comments: