Pages

Wednesday, February 27, 2013

MAANDAMANO YA MAJI KUFANYIKA TAREHE 16 MACHI


John Mnyika (Mb.) akiongea na wakazi wake waishio Goba.
Picha na Shabani Tolle

 Umati wa wakazi wa Goba wakimsikiliza mbunge wao, John Mnyika (hayupo pichani)
Picha na Shabani Tolle

Baadhi ya wakazi wa Goba wakifuatilia mkutano na mbunge wao kwa makini.
Picha na Shabani Tolle

(Na Shabani Tolle)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeazimia kufanya maandamano ya amani ili kuishinikiza serikali kutatua tatizo la maji hususani eneo la Goba ambalo linakabiliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu sasa.

Azimio hilo lilifikiwa hivi karibuni katika mkutano wa hadhara uliofanywa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo, Mhe. John Mnyika ambaye amesema kuwa azma hiyo imefikiwa baada ya serikali kushindwa kutimiza ahadi waliyotoa ya kumaliza tatizo hilo la maji kwa eneo hilo hadi kufikia tarehe 20 mwezi huu.

Aidha Mhe. Mnyika amefafanua kuwa maandamano hayo yatafanyika tarehe 16 mwezi ujao (Machi) na kwamba yeye mwenyewe ndiye atakayeongoza mandamano hayo.

Hivi karibuni, Waziri wa Maji Mhe. Profesa Jumanne Magembe aliahidi kumaliza tatizo la maji kwa wakazi wa Goba hadi kufikia tarehe 20 Februari katika mkutano wa hadhara na wakazi wa Goba.

No comments: