Pages

Thursday, February 21, 2013

BARABARA YA VINGUNGUTI-TABATA YAKARABATIWA

(Na Shabani Tolle)
Kufuatia kukarabatiwa kwa barabara ya Vingunguti ambayo inaunganisha maeneo ya Tabata na barabara kuu ya Nyerere inayoelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere na katikati ya jiji, watumiaji wa barabara hiyo wamepongeza jitihada ambazo zimefanywa na manispaa ya ilala kwa kukarabati barabara hiyo ambayo ni muhimu kwao.
Bw Julius Ngahyoma ambaye ni mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo, akizungumza na mwandishi wetu amesema “barabara hiyo hapo awali ilikuwa inapitika kwa shida kutokana na ubovu wake lakini  sasa inapitika vizuri na haina mashimo tena."   Ngahyoma ameiomba Manispaa kuhakikisha wanaiangalia mara kwa mara barabara hiyo kutokana na kwamba inatumiwa na watu wengi sana.
Aidha watumiaji hao wameshauri kuwa kutokana na barabara hiyo kutumiwa na watu wengi ni vizuri Manispaa ikaitengeneza kwa kiwango cha lami ili iwe madhubuti zaidi huku wakiongeza kuwa endepo itaachwa hivyohivyo mvua zitakapoanza kunyesha wana uhakika hali ya barabara hiyo itarudia tena kuwa mbaya.

Wamesema barabara hiyo kwa sasa ni mkombozi mkubwa hususani nyakati za asubuhi na jioni kutokana na watu wengi wanaoenda makazini kuitumia na hivyo kupunguza foleni kubwa ambayo imezoeleka katika maeneo ya Tabata.
 Magari yakipita kwa urahisi katika kilima kidogo kilichopo katika barabara hiyo.

Magari yakipishana kwa urahisi katika barabara hiyo (picha na Shabani Tolle)

No comments: