Pages

Thursday, March 15, 2018

WAZIRI SHONZA AFUNGUKA, AMTAJA ALI KIBA KUWA MFANO WA KUIGWA

Juliana Shonza, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amefunguka kufuatia sakata la  baadhi ya nyimbo za wasanii wa Bongo kufungiwa, amesema Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kuufanyia shoo nje ya nchi.

Amesema kuwa endapo msanii atafanya kitendo hiko atakuwa amekiuka sheria na kanuni za nchi.

”Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kufanyia shoo nje ya nchi ” amesema Shonza.

Aidha amewaasa wasanii nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa ufanisi na uweledi mkubwa ili kutokiuka sheria na taratibu za nchi kwa lengo la kuendeleza na kukuza muziki na maadili ya Tanzania.

Amewataka wasanii waige mfano wa mwanamuziki Ali Kiba ambaye amemsifia kuwa anaiwakilisha vyema nchi ya Tanzania kimataifa.

”Kwa mfano Ali Kiba, ni msanii mkubwa wa kimataifa ambaye anaiwakilisha nchi vyema, lakini haimbi nyimbo za lugha chafu wala hatengenezi video ambazo hazina maadili,” ameongezea Shonza.

Amesema Wizara yake inataka sanaa iende pamoja na ukuaji wa maadili ya nchi na amesisitiza wasanii kutoa burudani huku wakilinda tamaduni za nchi yao.

Shonza amefunguka hayo kufuatia sakata la baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva kufungiwa nyimbo zao kwa kukiuka kanuni na maadili.  Kufuatia sakata hilo, msanii Roma Mkatoliki alifungiwa kujihusisha na muziki kwa muda wa miezi sita kwa kutotii agizo la Naibu Waziri huyo.

No comments: