Pages

Thursday, March 8, 2018

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, MAGUFULI ASEMA HAYA KWA WANAWAKE:

Leo Machi 8, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika siku ya wanawake duniani amefunguka na kuwapongeza wanawake wote wa Tanzania na kuwatakia heri katika siku yao.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais Magufuli amesema wanawake wamekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii na kusema daima ataendelea kuwaheshimu.

“Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu,” Rais Magufuli .

No comments: