Pages

Friday, March 23, 2018

MGANGA AKAMATWA KWA KUSABABISHA MAUAJI TABORA

Mganga aliyekamatwa (mwenye nguo ya kijani) akiwa pamoja na vifaa vyake vya kazi anavyotumia kupiga ramli chonganishi iliyosababisha mauaji huko Ulyankulu Mkoa wa Tabora.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kumkamata  mganga wa Jadi mwenye kupiga ramli chonganishi na kusababisha mauaji ya mama mmoja aliyefahamika kwa jina la NDILU MBOGOSHI, Miaka 65, Msukuma, Mkulima, Mkazi wa Shilabela Kata ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora, ambaye aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani.

Mara baada ya tukio hilo  upelelezi ulifanyika na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora liliweza kubaini na kumkamata  mganga wa jadi huyo ambaye amefahamika kwa jina la THERESIA  PAULO, 57YRS, MSUKUMA, mganga wa jadi na mkazi wa  ISAGEGE-SASU Tarafa ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua.

No comments: