![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Wilbrod Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, asubuhi ya leo Februari 16, amewaapisha Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria.
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. |
ANGALIA VIDEO YA TUKIO ZIMA HAPA CHINI:
No comments:
Post a Comment