
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii
kutoka katika Mikoa na Halmashauri nchini na kusisitiza kuwa ana imani
nao katika kujenga uchumi wa Viwanda wakati akifunga Mkutano Mkuu wa 12
kwa Wataalm wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii uliofanyika kwa siku nne
katika Ukumbi wa Chuo cha Mioango Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
……………..
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.
Selemani Jafo ameeleza imani yake kubwa kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii
katika kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za Maendeleo
zitakazowezesha kufikia uchumi wa viwanda.
Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati
akifunga Mkutano wa 12 wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii
uliofanyika kwa siku nne katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango.
Mhe. Jafo ameeleza kuwa kama
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakitumika vizuri katika maeneo yao wataleta
mabadiliko yenye tija yatakayosaidia kufikia uchumi wa viwanda.
“ Nina imani na Maafisa Maendeleo
ya Jamii katika kutumia weledi walionao kufanikisha kampeni ya kitaifa
ya viwanda vyetu, mkoa wetu ambayo nimeizindua hapa mkoani Dodoma”
alisema Mhe. Jafo.
Mhe Jafo amefafanua kuwa Kampeni
hii imeanzishwa kwa lengo la kusisimua na uanzishaji wa angalau viwanda
100 kwa kila mkoa ndani ya jamii ya Tanzania ambao utasimamiwa na
Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kuamsha ari na kuipa kipaumbele katika
utendaji wao wa kila siku.
Ameongeza kuwa watanzania
wanamatarajio makubwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na Tanzania
ya viwanda na azma hiyo itaweza kufikiwa kupitia kwa Maafisa ya
Maendeleo ya Jamii ambao ni mawakala wa mabadiliko katika jamii zetu.
Mhe. Jafo amesisitiza kuthamini
kada ya Maendeleo ya Jamii na kuwaagiza wakurugenzi wa Halmashauri ambao
walishindwa kuleta watumishi wao kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Sekta
ya Maendeleo ya Jamii kujieleza kwake na watakuwa na jukumu la kutoa
taarifa ya kazi zilizofanyika chini ya utendaji wa Idara ya Maendeleo ya
Jamii.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga
amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kwenda kufanya kazi kwa hamasa
kubwa ili kuacha alama katika jamii kwa kuonesha matokeo mazuri ya kazi
zilizofanyika wakati wa utumishi wao kwa umma.
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wataalam
wa Maendeleo ya Jamii umemalizika Mjini Dodoma na kutoka na maazimio
muhimu yakiwemo kwenda kuleta mabadiliko kwa wananchi kwa kuamsha ari
yao ya kujishughulisha katika kujiletea Maendeleo yao na taifa kwa
ujumla ili kuwezesha kufikia uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment