Pages

Friday, November 24, 2017

KESI YA RUGEMALIRA NA SINGH YAAHIRISHWA HADI DISEMBA


KESI ya James Rugemalira na Harbinder Singh Sethi imeahirishwa hadi  Desemba 8 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

Kesi hiyo inasikilizwa na Mahakama ya Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi.

Wakati huohuo, upande wa utetezi umemueleza Hakimu kuwa unaomba upelelezi ukamilike kwa haraka kwa sababu hali ya mshtakiwa (Sethi) si nzuri.

Upande wa Jamhuri nao umedai kuwa unafahamu kuwa washtakiwa wana haki zao na ndiyo maana wanajitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati muafaka.
 

No comments: