![]() |
| Juhudi za kuopoa miili ya watu waliokuwemo kwenye gari hiyo zikifanyika. |
Zimepokelewa picha na maelezo kadhaa kutoka kwa mdau aliyeko jijini Mwanza zikionesha na kueleza kutokea kwa ajali jijini humo mapema leo.
Mdau huyo amesema kuwa ajali hiyo ni ya gari ndogo ya abiria aina ya Hiace ikiwa na ibiria, imepitiliza na kutumbukia ziwa Victoria katika kivuko cha kigongo feri -Busisi, Wilayani Misungwi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 8 na majeruhi wawili. Juhudi za kuopoa miili zinaendelea kufanyika.
Picha zaidi za tukio hilo hizi hapa chini:
![]() |
| Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio hilo la kuzama kwa gari ndogo ya abiria (HIACE) ambalo namba zake za usajili hazikuweza kutambulika mara moja mara baada gari hilo kuopolewa ziwani. |
![]() |
| Wananchi kutoka maeneo mbali mbali wakilifuatilia tukio hilo mapema leo Kigongo Feri jijini Mwanza. |
![]() |
| Gari linalosemekana kutumbukia ziwa Victoria leo na kusababisha vifo vya watu kadhaa. |
INNA LILLAH WAINNA ILAH RAJIUN...




No comments:
Post a Comment