
Na. Immaculate Makilika –MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na Rais wa Benki ya
Dunia, Dkt. Jim Yong Kim wanatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi
wa barabara za juu (Ubungo interchange) eneo la Ubungo jijini Dar es
Salaam Machi 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano inasema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika
makutano ya Ubungo yatagharimu takribani shilingi bilioni 188.71 ambapo
una lengo kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro,
Nelson Mandela na Sam Nujoma.
“Mradi huo ni sehemu ya
uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban
Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki
ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania”
Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa,
mradi huo utahusisha pia awamu ya tatu na ya nne ya ujenzi wa
miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit- BRT), katika
barabara ya Nyerere kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongo
la mboto na barabara ya Bagamoyo kutoka katikati ya jiji hadi Tegeta.
No comments:
Post a Comment