Pages

Tuesday, February 7, 2017

NYUMBA YA WEMA SEPETU YAPEKULIWA, AKUTWA NA BANGI

Tokeo la picha la picha ya wema sepetu

Mrembo Wema Sepetu anatarajiwa kupandishwa kizimbani kufuatia tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi katika nyumba anayoishi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amesema kuwa Wema na mwenzake watapandishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na bangi kwenye nyumba zao.

Kamanda Sirro alisema kuwa katika upekuzi uliofanywa katika nyumba ya Wema Sepetu, ulikutwa msokoto mmoja wa bangi pamoja na karatasi maalum za kuvutia bangi zijulikanazo kama 'rizla'.

Pamoja na Wema Sepetu, mwingine atakaepandishwa kizimbani ni pamoja na Bakari Mcheni ambaye yeye katika upekuzi alikuwa na misokoto mitatu ya bangi.

Kamanda Sirro alisema watu 10 watapelekwa mahakamani kwa ajili ya kula kiapo juu ya mwenendo wa kimaadili kutokana na kutumia dawa za kulevya ambapo kwa ndani ya miaka miwili wasihusike na kutumia dawa hizo pamoja na kuripoti Polisi mara mbili kwa mwezi.  Watu hao watakaokula kiapo hicho ni Hamidu Chambusao, Rumeo George, Sideo Mwandigo, Khalidi Mohamed 'TID', Johanes Mansen, Said Masoud 'Petit Man', Rajab Salum, Lulu Chelangwa, Nasoro, pamoja na Bakari Kierefu.

Katika operesheni hiyo ya kusaka watu wanaojihusisha na dawa za kulevya walikamatwa umla ya watu 112 ambapo kati yao 12 ni wasanii wa bongo fleva na bongo muvi.

Aidha katika operesheni inayoendelea, dawa za kulevya 299 na puli 104 vilikamatwa.

Akizungumzia madai kuwa kuna baadhi ya watu wameonewa, kamanda Sirro amesema kuwa watu wote waliokamatwa hakuna mtu aliyeonewa katika hilo na walikuwa wazi katika mahojiano.
Chanzo: Swahili times

No comments: