Pages

Friday, August 26, 2016

MSANII GABO ZIGAMBA AWATAHADHARISHA WANANCHI JUU YA UTAPELI KUTUMIA JINA LAKE



Msanii nguli wa Bongo movies, Gabo Zigamba
Wezi wa mtandaoni wameonekana kutembea karibu na msanii nguli wa Bongo Movies, Gabo Zigamba ikiwa ni siku chache tangu walipoidukua akaunti yake ya facebook.

Msanii huyo ametoa tahadhari kuhusu utapeli unaoendelea kwa kutumia jina lake.

Awali, msanii huyo alipoteza simu mbili za mkononi ambazo baadaye zilionekana kutumiwa na matapeli hao kuomba msaada kwa watu mbalimbali wakijifanya kuwa wao ndio Gabo.

Kadhalika, juzi akaunti ya Facebook ya msanii huyo ilidukuliwa na kutumiwa kwa muda na matapeli hao kwa kujifanya ndio msanii huyo.  Hata hivyo, hatimaye alifanikiwa kuirejesha akaunti hiyo katika himaya yake.

"Nahisi mimi ndio msanii ninayeongoza kwa jina langu kutumiwa na matapeli kwa sababu nimekuwa nikipata taarifa mbalimbali kuhusu watu wanaolitumia," amesema Gabo na kuongeza:

"Kwa mfano kuna binti mmoja aliyejifanya yeye ni Gabo na amekuwa akitapeli kwa kudai anauza mabegi."

Msanii huyo ametoa wito kwa watanzania kuwa makini na watu wanaotumia majina ya watu wengine, hususan wale maarufu kwa minajili ya kuwatapeli.

Amesema kuwa yuko kwenye mchakato wa kufungua akaunti zake mpya za mitandao ya kijamii.

No comments: