Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe Mwigulu Nchemba alipomtembelea mmoja wa majeruhi wa tukio hilo. |
Waziri Nchemba akiwa nje ya eneo la tukio. |
Inasemekana tukio hilo limetokea mnamo saa 1.30 usiku wakati askari hao wakibadilishana lindo katika benki hiyo na ndipo ghafla wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kuanza kuwashambulia kwa risasi.
Askari waliofariki wametajwa kuwa ni E5761 CPL Yahaya, F4660 CPL Hatibu na G9544 PC Titto.
Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo ambapo mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.
Inadaiwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki.
Gari la Polisi (Leyland Ashok) lililokuwepo eneo hilo pia limeharibiwa kwa risasi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amethibitisha kuwepo na tukio hilo. "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi hapa Mbagala lakini taarifa kamili ntazitoa kesho kwa kuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi" alisema Sirro.
ALICHOSEMA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MHE. MWIGULU NCHEMBA - 23.08.2016
"Usiku huu nimefika Mbagala Mbande wilaya ya Temeke, eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo. Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili, nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri. Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya, natoa rai kwa wahusika kujisalimisha. Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu." 23.08.2016
Chanzo: Michuzi Blog

No comments:
Post a Comment