Mahakama Kuu kanda ya Iringa imemhukumu miaka 15 jela kwa kosa la kuua bila kukusudia askari wa kikosi cha kuzuia ghasia, pacifius Simon aliyekuwa akituhumiwa kumuua mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi huko Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Hukumu hiyo iliahirishwa toka wiki iliyopita hadi leo ambapo Jaji wa Mahakama hiyo, Dk Paul Kihwelo amesema kuwa Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo kufuatia ushahidi alioutoa mlinzi wa amani.
Jaji Kihwelo amesema kuwa mbele ya mlinzi wa amani, mtuhumiwa alikiri kosa hilo akisema alitenda bila kudhamiria.

Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment