
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
Kamati Maalum iliyoundwa kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu
wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015
imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.
Akizungumza Katika kikao cha
Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa niaba ya Wajumbe
wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya
majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa.
Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume
imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ikiwa ni
pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa lengo ni
kuhakikisha kuwa taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema
mwezi Julai mwaka huu.
Pongezi hizo pia zimetolewa na
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Ramadhan
Kailima wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo muda mfupi baada ya
kumalizika kwa mkutano wa Tume akieleza kufurahishwa kwake na namna
ambavyo dhana ya ushirikishwaji ilivyotumika katika kuandaa Rasimu hiyo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
iliratibu na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kuanzia Otoba 25
mwaka jana na kuhitimisha rasmi zoezi hilo Machi 20 mwaka huu kwa
Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele mkoa wa Kaskazini Unguja.
No comments:
Post a Comment