Pages

Sunday, May 1, 2016

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF, WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI KWA MARA YA KWANZA



 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi yakilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani  (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF, kwa mara ya kwanza umeshiriki kwenye matembezi ya kusherehekea siku ya Wafanyakazi, maarufu kama MAY DAY jijini Dar es Salaam leo Mei 1, 2016.

Matembezi hayo yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi, ambazo ndio wadau wakubwa wa Mfuko huo, yalianzia kwenye ofisi za Shirikisho la Vyamavya Wafanyakazi, TUCTA, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kupita barabara ya Nkurumah, Nyerere na kisha kupinda barabara ya Chang’ombe hadi uwanja wa Uhuru ambako yalipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.

WCF ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.

Tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, juhudi za kutangaza hudumazake kwa wadau zimekuwa zikiendelea mfululizokwa kutoa elimu kupitia semina, maonyeshona makongamano   lakini pia kupitia vyombo vyahabari na kwa siku ya Mei Day imekuwa ni fursa kubwa ya WCF kuungana na wadau wake wakubwa.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi ya kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani  (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.
 Wafanyakazi
wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya
kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani
 Matembezi yakiwa yameingia Uwanja wa Uhuru
 Matembezi yakipita barabara ya Chang’ombe
 Matembezi yanaendelea, hapa ni barabara ya Uwanja wa Taifa  mkabala na ofisi za TAKUKURU wilaya ya Temeke
 Matembezi yakiendelea barabara ya Chang’ombe
 Matembezi yakiwa barabara ya Uwanaja wa Taifa
 Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye matembezi hayo, hapa nibarabara ya Chang’ombe
 Baadhi
ya wafanyakazi wa WCF, wakimsikiliza mwenzao aliyevaat-shirtyenye ujumbe maalum
wa Mfuko huo “WCF inatoa Fidia Stahiki kwa Wafanyakazi wote wa Sekta ya Ummana
Binafsi”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam, Mh. Paul Makonda, (kulia), akiteta jambo na kiongozi
wa Shirikisho la Wafanyakazi mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kilele cha May
Day uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Nyuso za furaha baada ya matembezi

No comments: