Pages

Tuesday, August 12, 2014

SIMBA WAMTIMUA KOCHA WAO MKUU


SIMBA wamemtimua Kocha wao Mkuu, Mcroatia Zdravko Logarusic, ikiwa ni baada ya juzi kufungwa mabao 3-0 na Zesco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya maadhinisho ya Tamasha la klabu hiyo maarufu kama 'Simba Day' linalofanyika kila mwaka.

Logarusic ametimuliwa baada ya Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kukutana jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tangu aliposaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo.

Habari za kutimuliwa kwa Logarusic pia zimethibitishwa na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar akisema kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na tabia ya kocha huyo kutokwenda na falsafa ya klabu yao.

No comments: