Aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi wa Rwanda katika miaka ya 1994 hadi 2004, Patrick Karegeya amekutwa amefariki usiku wa Jumatano nchini Afrika Kusini.
Mwili wake ulikutwa katika chumba cha moja ya hoteli kubwa za mjini Johannesburg iitwayo Mihaelangelo. Chama chake cha RNC kinatuhumu utawala wa Rwanda kuhusika na kifo chake.

Kigogo huyo wa zamani wa Rwanda alikuwa mpinzani mkuu wa utawala wa Rwanda na alikimbilia nchini Afrika Kusini toka mwaka 2007. Awali alikuwa mshirika wa karibu na rafiki wa Rais Paul Kagame.
Kwa mujibu wa polisi nchini Afrika Kusini, vipimo vya macho baada ya kuuwawa vimeanzishwa ili kujua waliohusika na kifo chake.
Awali vyanzo vya habari vilifahamisha kwamba Patrick Karegeya alinyongwa kutokana na shingo ya mkuu huyo wa zamani wa idara ya ujasusi wa Rwanda kukutwa na uvimbe na kulikuwa na kamba iliyokotwa kwenye eneo la tukio.
“Alikodi chumba tarehe 29 mwezi Desemba, lakini asubuhi ya Alhamisi polisi ilikuta mwili wake umelazwa kwenye kitanda. Uchunguzi wa kwanza unaonyesha kuwa shingo yake ilinyongwa na kumeokotwa ndani ya chumba alichokuwa amekodi kamba na fulana ambayo ilikuwa na damu, ikimaanisha kuwa amenyongwa”, amesema Katlego Mogale, msemaji wa polisi nchini Afrika Kusini, akibaini kwamba vipimo hivyo vitaonesha ni muda gani kifo chake kilitokea.
Katlego Mogale, amesema wameanza kufanya uchunguzi wa kujua kwa nini alikodi hoteli hiyo na watu wangapi walikuwa ndani ya chumba chake.
“Timu ya wachunguzi inatathmini kwa sasa picha zilizorekodiwa na kamera za ulinzi”, amesema Katlego Mogale.
Mchana wa tarehe 31 Desemba, Patrick Karegeya alimfahamisha mmoja kati ya watu aliokutana nao kwamba ataonana kwa mazungumzo na rafiki yake wa muda mrefu anaejulikana kwa jina la Apollo Ismael Kiririsi, jioni ya siku hiyo kwenye hoteli ya Michelangelo Towers.
Jamaa zake waliwasiliana naye mara ya mwisho saa moja na nusu usiku, na toka muda huo mawasiliano kati ya mkuu huyo wa zamani wa idara ya ujasusi nchini Rwanda na jamaa zake yalikosekana.
Jamaa na marafiki wa Patrick Karegeya nao pia wanautuhumu utawala wa Rwanda kuhusika na kifo hicho.
Awali mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, Jenerali Kayumba Nyamwasa aliye ukimbizini nchini Afrika Kusini, ambaye pia alinusurika kuuwawa katika mazingira kama hayo mwaka 2010, amesema kwamba ni mauwaji ya kisiasa.
“Sina shaka na tukio hili, serikali ya Rwanda inahusika na kifo cha Patrick Karegeya. Marehemu hakuwa na ugomvi na mtu yeyote hapa Afrika Kusini, isipokua Rais Paul Kagame, ambaye alimfuatila ili amuangamize kwa kipindi chote hiki cha miaka kumi iliyopita. Haya ni mauwaji ya kisiasa, kama jinsi serikali ya Rwanda imekuwa ikifanya kwa wapinzani wake”, amesema Jenerali Kayumba Nyamwasa.
Patrick Karegeya aliwahi kumshutumu Rais Paul Kagame kwamba alipanga njama ya kuilipua ndege aliyokuwemo mtangulizi wake, Rais Juvenal Habyarimana, akilaumu kwamba, Paul Kagame ndiye mwanzilishi wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.
Duru za Kidiplomasia kutoka Rwanda zinafahamisha kwamba Serikali ya Rwanda haijatoa tangazo lolote linalohusiana na kifo hicho, kwani kesi hiyo iko mikononi mwa vyombo vya sheria vya Afrika Kusini.

CHANZO: RFI Kiswahili
No comments:
Post a Comment