Pages

Monday, December 16, 2013

WAKAZI WA KEKO MAGOROFA YA NHC WAPINGA KUHAMISHWA KATIKA NYUMBA HIZO


BOFYA HAPA UPATE HABARI LIVE

JESHI LA POLISI MKOA WA TEMEKE HIII LEO WAMEFANIKIWA KUZUIA MAANDAMANO YA WAKAZI WANAOISHI NYUMBA ZA SHIRIKA LA NYUMBA TANZANIA-NHC ZILIZOPO ENEO LA KEKO JIJINI DAR ES SALAAM AMBAO WALIAZIMIA KUANDAMANA MPAKA MAKAO MAKUU YA SHIRIKA HILO KWA LENGO LA KUPINGA NOTISI WALIZO PEWA ZA KUSITISHA MKATABA WA UPANGAJI WAO MPAKA IFIKAPO MWISHONI MWA MWEZI MEI 2014.

ITV MARA BAADA YA KUWASILI ENEO HILO LIMEWAKUTA WAKAZI HAO WAKIWA WAMEJIKUSANYA NJE YA MAGOROFA HAYO WAKIWA WAMEBEBA MABANGO BILA KUJUA WAENDE WAPI BAADA YA KUSITISHWA KWA MAANDAMANO HAYO AMBAPO WAMELALAMIKIA SHIRIKA HILO KUWA HALIJA WATENDEA HAKI KWA KUWA HAWAJUI KWA NINI WANAHAMISHWA ANGALI BAADHI YAO WAMEKAA KATIKA NYUMBA HIZO KWA ZAIDI YA MIAKA 40 SASA NA KUKITAJA KITENDO HICHO NI CHA UNYANYASAJI NA HIVYO KUIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI.

MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WA SHIRIKA HILO BI SUZAN OMARI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA SAKATA HILO AMEKIRI KUWA SHIRIKA HILO LIMETOA NOTISI YA MIEZI SITA KWA WAPANGAJI WA BLOCK C,F,G NA H NA KUFAFANUA KWAMBA SABABU KUU YA KUTOA NOTISI HIZO NI KWAMBA UMILIKI WA NYUMBA HIZO UTABADILIKA NA KUWA CHINI YA TAASISI MOJAWAPO YA SERIKALI AMBAPO UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA ARDHI YA MWAKA 1999 INAMTAKA MMILIKI KUTOA NOTISI YA SIKU 30 KWA MPANGAJI WAKE KABLA YA KUMUHAMISHA.

NAYE MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA ENEO HILO AMESEMA KUWA KAYA ZAIDI YA 64 PAMOJA NA WATEGEMEZI WAO WANAISHI KATIKA MAGOROFA HAYO AMBAPO BAADHI YAO NI WAJANE, WALEMAVU NA WENGINE NI WAASTAAFU NA HAWAJUI WAKITOKA KATIKA NYUMBA HIZO WANAENDA KUISHI WAPI. 

No comments: