Pages

Monday, April 10, 2017

WATU WANNE KIZIMBANI KWA KUJIPATIA MILIONI 700 ZA UDANGANYIFU

Watu wanne wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka matatu likiwamo la kula njama, kutakatisha fedha na kujipatia dola 320,000 kwa njia ya udanganyifu ambazo ni sawa na shilingi milioni 704.

Akiwasomea hati ya mashtaka leo, Wakili wa Serikali, Esterzia Martin kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Deogratius Masika (40), William Kimonge (34), Yusuph Sabo (27) na Elladius Tesha (47).

Wakili huyo amedai kuwa kati ya Oktoba 2016 na Januari 2017 jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walikula njama ya kutenda makosa ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alidai kuwa kati ya Desemba 2016 na Januari 2017 washtakiwa hao walijipatia dola 320,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 704 za kitanzania baada ya kujifanya watasambaza tani 5,000 za korosho kutoka Mtwara kupitia kampuni ya SMCI America LLC ambayo ipo Marekani wakati wakijua ni uongo.

No comments: