Pages

Tuesday, April 11, 2017

MTANZANIA APORWA SHILINGI MILIONI 13 INDIA

NEW DELHI, India.  Mtanzania (65) ambaye jina lake halijafahamika, ameporwa mkoba wenye dola za kimarekani 6,000 (sawa na shilingi milioni 13.4) akiwa nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu ya mjukuu wake.

Fedha alizoporwa ni kwa ajili ya matibabu ya mjukuu wake aliyelazwa jijini New Delhi, India, gazeti la mtandaoni la The Times of India limeripoti leo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mwanamke huyo akiwa na familia yake aliporwa mkoba wake na watu wawili wakati akielekea hoteli iliyopo maeneo ya Karol Bagh, katikati ya jiji la New Delh, Ijumaa wiki iliyopita.

No comments: