Raisi wa Uganda, Yoweri Kaguta
Museven amelaani mauaji ya Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda
ambaye pia alikuwa ni Naibu Mkuu wa Jeshi hilo, Andrew Kaweesi na
walinzi wake wawili ambao walishambuliwa kwa risasi na watu
wasiojulikana katika eneo la Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa
mji mkuu Kampala, Nchini Uganda jana.
Bado
haijajulikana sababu hasa ya kutekelezwa mauaji hayo ingawa serikali
imeagiza kufungwa kwa kamera za usalama katika miji mikubwa yote nchini
humo wakati huu uchunguzi ukifanywa.
Katika kipindi cha miaka saba iliyopita takribani matukio ya mauaji 12 yametekelezwa na washambuliaji waliokuwa wakiendesha pikipiki maarufu kwa jina la boda boda ambao walitoroka eneo la tukio na kutopatikana licha ya jitihada za polisi kuendelea kufanyika kuwatafuta.
Kwa mujibu wa Luteni Jenerali, Henry Tumukunde, mara nyingi vitendo hivi hufanyika kwa umakini kujiamini na ujasiri huhakikisha wameua kabisa kabla ya wauaji kutokomea.

No comments:
Post a Comment