Pages

Monday, March 13, 2017

HIVI NDIVYO HALI HALISI ILIVYO DSM BAADA YA MVUA KUNYESHA LEO

Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam leo, soko la Sinza limelazimika kufungwa kwa muda kutoka na kujaa maji eneo lote la soko hilo.
Barabara nyingi za Dar leo zimejaa maji, hali inayopelekea magari mengi  kuzima, kama ionekanavyo pichani hapa.
Afande akitafakari jambo kufuatia uwingi wa maji katika barabara ya Bagamoyo eneo la Mbezi beach Goigi jijiji Dar es Salaam leo.
Wadau wakifanya mambo katika moja ya chemba iliyoziba kutokana na wingi wa uchafu uliokuwa umesombwa na maji hayo.
 Magari yote yamelazimika kupita upande mmoja wa barabara kutokana na wingi wa maji upande mwingine.

No comments:

Post a Comment