……………………………………………………………………………………….
Na Daudi Manongi-WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa
Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa
ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi
nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo
kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa
shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.
Mhe.Wambura alisema hayo wakati
alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo
aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011
mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo
ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati
miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
“Taratibu za Kisarawe za
upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa
kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba
kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa
lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za
Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu,” alisema Mhe Wambura.
Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo
kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa
mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au
kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya
kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye
hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi kubomoa nondo
na kuuza kama vyuma chakavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)
Bi.Joselin Lugola alimwahidi Waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye
bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa na kudai kwamba
mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza
ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa
hiyo hata za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.
No comments:
Post a Comment