Pages

Wednesday, May 25, 2016

MTOTO ALIYEPOTEA AKUTWA AMEKUFA KATIKA CHEMBA YA CHOO, DSM

IMG_20160524_165755
Mwili wa mtoto Kelvin kama ulivyokutwa katika chemba hiyo maeneo ya Manzese, DSM.
IMG_20160524_175452
Gari la Polisi likiwa limewasili eneo la tukio.

Mtoto mmoja anayefahamika kwa jina la Kelvin (2) amekutwa amekufa katika chemba ya choo baada ya kupotea kwa siku mbili na kutafutwa na wazazi wake bila mafanikio.

Tukio hilo lilitokea Jumanne ya Mei, 24 katika eneo la Manzese, Mferejini ambapo mashuhuda wanaomfahamu mtoto huyo walisema kuwa alipotea siku ya Jumapili Mei, 22 na kutafutwa na wazazi wake bila mafanikio.

“Kuanzia Jumapili anatafutwa hajapatikana wakaenda hadi kutangaza msikitini na taarifa ikarushwa ITV kuhusu kupotea kwake lakini hakukuwa na mafanikio yoyote,” mmoja wa mashuhuda aliiambia Mo Blog.

IMG_20160524_180225
Magari ya uokoaji yakiwa eneo la tukio.
Alisema kuwa kupatikana kwa mtoto katika chemba ya choo ni baada ya fundi ambaye alitakiwa kujenga chemba hiyo ambayo ilikuwa imefunikwa na mabati na alipofungua ndipo alipokuta mtoto akiwa ndani ya chemba hiyo.

Baada ya kuona hivyo, fundi huyo ambaye ni ndugu na mmiliki wa nyumba alitoa taarifa kwa uongozi wa mtaa ambao walitoa taarifa kwa vyombo vya usalama ikiwemo Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto ambao walifika eneo la tukio na kumtoa mtoto katika chemba na kuondoka nae.
IMG_20160524_180528
Mwili wa mtoto Kelvin ukiingizwa katika gari la Polisi.
IMG_20160524_180540

Aidha taarifa zingine zinaeleza kuwa hadi tukio hilo linatokea mama wa mtoto alikuwa kanisani katika maombi ya kumuombea mtoto wake na baba wa mtoto akiwa nyumbani ambaye alionekana kushtushwa na hali aliyoiona kwa mtoto wake na hivyo wasamalia wema wakamtoa eneo la tukio na kumpeleka nyumbani ili kumtuliza na tukio hilo ambalo limemtokea mtoto wake.
Chanzo: Mo Blog
Picha mbalimbali za mashuhuda wakifuatilia tukio hilo:
IMG_20160524_175458
IMG_20160524_175830
IMG_20160524_180614

No comments: