Pages

Thursday, May 5, 2016

MSANII SNURA AOMBA RADHI WATANZANIA BAADA YA WIMBO WAKE WA 'CHURA' KUFUNGIWA

Msanii Snura Mushi (kulia) akiwa na Meneja wake, Hemedi Kavu.
Baada ya jana Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuufungia wimbo wa Snura 'Chura' mpaka atakapo ufanyia marekebisho, leo tarehe 5 Mei 2016 Snura Mushi amewaomba radhi Watanzania kwa kutoa wimbo huo ambao umesitishwa na Wizara ya Habari baada ya kuonekana kuwa wimbo huo una udhalilishaji na haupo katika maadili ya kitanzania.

"Tumewaita Waandishi wa habari kwa ajili ya kuomba radhi kwa Umma na Watanzania kwa ujumla kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mtandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya Kitanzania ya muziki unaoitwa Chura. Tunaviomba radhi vyombo vya Serikali vinavyosimamia sekta ya Sanaa kwa kutofuata sheria,kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji sanaa nchini, mimi na Meneja tunaahidi kutorudia tena kufanya tukio hilo la udhalilishaji na iwapo tutarudia basi tupewe adhabu kali kwa mujibu wa sheria za nchi hii."

Msanii Snura Mushi akiwa na Meneja wake.

Snura
Msanii Snura Mushi akionesha waandishi wa habari Cheti chake alichopata baada ya kusajiliwa na BASATA.
Serikali ilipiga marufuku maonyesho yote ya hadhara ya Snura hadi pale atakapokamilisha usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Akizungumza na wanahabari akiwa ameandamana na meneja wake, Snura amesema amechukua hatua na kusajiliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kisanii.


 Tazama video ya Snura akiongea na waandishi wa habari:

No comments: