…………………………………………………………………………………………………….
SERIKALI ya awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria kuwa Serikali ya
mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.
Rais Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda.
Wakati Serikali ikisisitiza
kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti kupitia Ilani ya Chama cha
Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono hilo kila mmoja amekuwa na
kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo hilo.
Abdallah Ulega ni Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwa upande
wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha dhamira na kiu ya
kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo kuwa na viwanda.
Anasema kuwa lazima wao kama
wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge wanaotokana na Chama cha
Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi haya kwani wameahidi
hivyo lazima watende.
Ulega anasema kuwa Jimbo la
Mkuranga ni kubwa na linarutuba ya kutosha hivyo anakaribisha
wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda vidogovidogo na vikubwa
katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali Kwa ajili ya maendeleo ya watu
wake.
Anasema kuwa kuna jitihada kama
Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba jimbo lake ni miongoni
mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya Serikali ya kutaka mageuzi
ya viwanda.
“Kimsingi jimbo langu la Mkuranga ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo maana naomba wahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda.”anasema ulega
Anasema kuwa kutokana na utajili
wa Ardhi yenye rutuba wanaweza kujenga viwanda vya kusindika mazao
lakini pia kwa sababu eneo lao ni kubwa basi hata viwanda vya kubangua
korosho na kujengwa Kwa viwanda hivyo kutasaidia kuleta ajira katika
eneo hilo.
Anasisitiza kuwa ndio maana
wakati akichangia mpango wa wa maendeleo wa Serikali Kwa miaka mitano
ameomba Serikali na wahisani kujitokeza Mkuranga lakini Kwa upande wa
Serikali kuiweka Mkuranga kuwa sehemu yenye hitaji la ujenzi wa viwanda.
Anasema amebainisha wazi kiu ya wananchi wa jimbo lake la kutaka maendeleo na ajira hivyo bila kuwepo na viwanda hakuna ajira inayoweza kuwepo na zaidi vijana watazidi kulaumu serikali yao.
“Nimesema wazi kuwa Mkuranga
kuna matatizo ya miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara.Maji .kilimo na
mambo mengine na katika baadhi ya maeneo haya nashukuru baadhi ya
marafiki wameitikia mwito wangu na wameweza kusaidia katika kichimba
visima ambapo wananchi wangu wameaza kupata Maji safi na salama.”anasema
Ulega
Anasema kuwa anawashukuru
African Foundation Reflection Kwa kuonesha moyo wa kusaidia na juhudi
hizo zote zimetokana na jitihada zake za kutaka kuona siku moja Mkuranga
inakuwa ya kutolea mfano tofauti na ilivyo sasa.
Aidha katika mpango huo wa
maendeleo Kwa miaka mitano Kwa Serikali ameomba kujengewa barabara
Kutoka Kisiju hadi Mkuranga Kwa kiwango cha lami kwani barabara hiyo ni
muhimu Kwa wananchi wa wilaya hiyo lakini hata wale wanaotoka Mafia.
Pia anasema katika mpango
mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano Kuhusu maendeleo ya
miundombinu nchini na hapo aliangalia wilaya ya Mafia kwa sababu pale
kuna bandari na watu wake pia ndiyo wazalishaji wakubwa wa korosho na
samaki.
Anasema kuwa pia kwenye kata
yake ya mbezi kwaniaba ya wananchi wake wa Mkuranga wangeishauri
Serikali kuwa eneo la viwanda ili wananchi wake wawe sehemu ya
uzalishaji wake.
Aidha Ulega anazungumzia suala
la kuondoa kero ya uhaba wa upatikani wa Maji katika jimbo hilo ambapo
Serikali ingefanya bidii ya kutoa maji hayo kutoka katika mto rufiji
kupitia kibiti hadi kufika Mkuranga na hatimaye Dar es Salaam.
Anasema haiwezekani Kwa miaka
nenda rudi tatizo la Maji halipatiwi ufumbuzi wakati Mkuranga inapitiwa
kwa karibu na Mto Rufiji ambapo mikakati madhubuti ya kuleta Maji
ikifanyika tatizo hilo litabaki kuwa historia katika eneo hilo.
Anasema tatizo la ajira Kwa
vijana ni kubwa mno hivyo wanashukuru Serikali Kwa kutambua umuhimu wa
kutilia mkazo uazishwaji na ufufuaji wa viwanda kwani eneo hilo ndilo
linaweza kuwa.msaada Kwa vijana kuweza kupata ajira.
“Mimi kama Mbunge wao kama
nilivyosema awali nitaendelea kupambana na kufanya kila linalowezekana
Kwa kuhakikisha Mkuranga inakuwa sehemu ya viwanda na naendelea kitoa
rai Kwa wawekezaji kuchangamkia Ardhi yetu Kwa kujenga viwanda vingi ili
vijana wangu wapate ajira.”anasema
Anaongeza kuwa mkuranga
ilisahaulika mno pamoja kwamba ni miongoni mwa wilaya za siku nyingi
lakini imekuwa nyuma kimaendeleo hivyo niwakati mwafaka wa kushirikiana
Kwa pamoja Kwa ajili ya maendeleo.
Anasema kuwa wananchi wake
waendelee kumuombea Kwa Mungu na wazidi kudumisha Umoja na mshikamano
ili Kwa pamoja wapambane Kwa lengo la kuona jimbo la mkuranga linakuwa
la mfano.
Akizungumzia kilimo cha korosho
anasema kuwa pamoja na zao hilo kuwa ndio zao linalotegemewa kuendesha
maisha ya wananchi wake lakini bado kwasababu ya ukosefu wa kuwepo Kwa
viwanda hususani vya ubanguaji kunafanya pasiwepo na tija sana
wanayoipata wananchi wake katika kilimo hicho.
Anasema kuwa kutokana na hali
hiyo ana kazi kubwa ya kuendelea kuzungumza na watu mbalimbali ili
kuleta ushawishi wa kukubali Kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda hivyo.
Pia akizungumzia Elimu anasema
anatambua changamoto zilizopo katika eneo hilo hivyo amedhamiria Kwa
dhati Kwa kushirikiana na Halmashauri wanaongeza hamasa Kwa wanafunzi
ili waweze kufanya vema katika masomo yao na hatimaye kuweza kupata
wataalamu wa baadae.
“Najua kuna Changamoto ya
madawati na hili tunalishugulikia Kwa kushirikiana na kamati mbalimbali
za Shule,wazazi,pamoja na walimu ili kuona namna ya kukabiliana na
tatizo hilo na hata uchakavu wa majengo .”anasema Ulega.
Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja
kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais
Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
No comments:
Post a Comment