|
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliongoza kikosi cha wananchi na maafisa wa wanyama pori kumsaka Kiboko aliyevamia mazao ya wananchi na kutishia maisha ya wananchi hao wa kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo. |
Kiboko huyo alijificha kwenye eneo ambapo wananchi wa kijiji hicho waliogopa kutembea kufanya shughuli za kilimo. mnamo saa 10 na nusu jioni kiboko huyo alipatikana na kuuawa na baadae wananchi kugawiwa nyama yake.
Ilikuwa kazi ngumu kumtoa kwenye dimbwi alilo angukia baada ya kuuawa kwa risasi. Kumekuwa na matukio ya wanyama wa porini kuvuka mbuga na kuingia vijijini. wiki mbili zilizo pita simba alionekana kijiji cha Idodi
|
Mmoja wa Maafisa Wanyama pori akitoa maelezo kwa wananchi kabla ya kwenda kufanyika kwa zoezi la kumdhibiti Kiboko huyo. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiwa ameambatana na baadhi ya wananchi na Maafisa Wanyama Pori kuelekea aliko Kiboko huyo. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo wakati wa kumtoa Kiboko huyo baada ya kuuliwa. |
No comments:
Post a Comment