Pages

Tuesday, September 10, 2013

KIWANDA CHA KWANZA CHA KUCHAMBUA TAKA (KIKUTA) CHAZINDULIWA GONGOLAMBOTO, DSM

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na wakazi wa Gongo la Mboto wakati alipotembelea na kukagua Kiwanda cha Kuchambua Taka (KIKUTA) kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar.

Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kuznugmza na wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto.
MANISPAA ya Ilala katika Kata ya Gongo la Mboto imezindua kiwanda cha kuchambua taka chenye uwezo wa kutengeneza Mbolea, Mboji na bidhaa mbalimbali zitokanazo na taka ngumu na nyepesi.
Kiwanda hicho awa kilijulikana kama kituo cha kutupia taka (KIKUTA) ambacho kilijengwa na mfadhili Bremen Overseas Research and Development kutoka Canada.
Kiwanda hicho cha kipekee kimetokana na juhudi za wakazi wa Gongo la Mboto na Kikundi cha Gongo la 
Mboto Youth Group wakisaidiana na viongozi wao na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Kiwanda hicho kitatoa ajira kwa vijana ili kujikwamua kwenye lindi la umaskini.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na wakazi wa Gongo la Mboto, amempongeza Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Meya wa Halamshauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwa jitihada zake za kuhamasisha usafi kwenye Manispaa yake na kuzitaka Manispaa zingine kuiga mfano wa Manispaa ya Ilala ambapo pia amewahamasisha wakazi wa Gongo la Mboto kutunza Mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na manadiliko ya tabianchi yanayopelekea ongezeko la Joto duniani.
Picha mbalimbali za tukio hilo:



 Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiangalia maji ya michoro iliyopo katika kiwanda hicho
inayohamasisha suala utunzaji wa Mazingira majumbani.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akipata maelezo kutoka
kwa mmoja wa wafanyakazi kiwanda hapo namna wanavyotengeza Mbolea
 kwa kutumia taka zilizooza.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akikagua kifaa
kinachotumika kuchambulia taka kwa ajili ya kuzalishwa upya kiwandani hapo.
 Mratibu wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and Development Bi. Larissa Duma (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) alipotembelea na kukagua kiwanda cha KIKUTA. Kushoto ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto na
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
   Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ,
Jerry Silaa pamoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA).
Source: wavuti.com

No comments: