Pages

Friday, August 23, 2013

KUMBUKUMBU YA BABA YETU MZEE ISAIAH AMON MWAIPAJA



23/08/2008 – 23/08/2013


Baba yetu mpendwa, leo tarehe 23/08/2013 unatimiza miaka mitano (5) tangu utwaliwe na Bwana mwaka 2008.

Sisi wanao Tony, Ipyana, Ivan na Irene, mama yetu Esther Victoria, wajukuu zako (Ben, Lulu, Baraka, Dan, Vicky, Milka & Vicent), wakwe zako pamoja na ndugu na wanaukoo wote bado tunakukumbuka kwa Busara na Upendo wako.

Tunajua kuwa kimwili haupo nasi ila tunaamini kuwa kiroho upo nasi.  Tunaendelea kujivunia na kuyaenzi mema uliyotufundisha enzi za uhai wako.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi. AMEN.

No comments: