Pages

Tuesday, August 27, 2013

KAMBI MISS TZ 2013 YAANZA RASMI "WAREMBO WAKUTANA NA WANAHABARI"





Warembo 30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2013, kesho wanatarajiwa kukutana rasmi na waandishi wa habari, ili kila mmoja kutoa mtazamo wake,shughuli itakavyofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi,jijini Dar es Salaam.

Akizungumzana waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino ambao ni waandaaji wa Redd’s Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema, mkutano katiya waandishi wa habari na warembo ni muhimu kuwajengea uwezo zaidi wa kujiamini.

“Washiriki hao wataulizwa maswali mbalimbali na waandishi wa habari na wao wataeleza mtazamo wao kuhusu Redd’s Miss Tanzania, hatutawafunga, wao 
waandishi watakuwa huru kila mmoja kumuuliza mshiriki yoyote swali analotaka,” alisema.

Washiriki hao ambao leo walikuwa na semina maalumu na waandaaji wa mashindano haya ambao ni Kampuni ya Lino International Agency Limited.

Baadaya kukutana na waandishi wa habari, warembo hao wanatarajiwa kuanza ziara maalumu ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa 
lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.

Warembo hao watakuwa kambini kwa muda wa siku 30 wakipata mafunzo mbalimbali yatakayotolewa na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali kama vile afya, ajira, ujasiriamali, uwekezaji na sekta ya utalii.

Brigitte Alfred ndiye Mrembo anayeshikilia taji hilo kwa sasa, baada ya kufanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.

Menejawa Redd’s, Victoria Kimaro naye alisema kama wadhamini wapo tayari kuhakikisha shindano hilo linafanikiwa zaidi mwaka huu kuliko kipindi 
kupita miaka ya nyuma.

Kinywaji cha Redd’s Original kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).


No comments: