Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiandika maelezo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa, wakati alipokuwa akichangia mada juu ya mustakabali wa amani na usalama wa taifa kwa miaka 50 ijayo. Kongamano hilo lilifanyika jana katika ukumbi wa Nkrumah uliopo UDSM.
Waziri Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo lililofanyika jana katika ukumbi wa Nkrumah jijini Dar es Salaam.
Waziri Nchimbi (wa pili kushoto) akifurahi jambo wakati alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa mara baada ya kufungwa kwa Kongamano hilo la Amani na usalama wa taifa kwa miaka 50 ijayo.
No comments:
Post a Comment